SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

KARIBU BUKOBAWADAU BLOG

SADATH BOUTIQUE

KABAGO SHOP

PROAKTIV COMMUNICATIONS

25 February 2017

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Akutana na Rais wa Ivory Coast Mheshimiwa Alassane Ouattara jijini Abidjan

Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jana tarehe 23Februari 2016 amekutana na kufanya mazungumzo  na Rais wa Ivory Coast, Mhe. Alassane Ouattara katika Ikulu yake jijini Abidjan.. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Makamu wa Rais, Waziri wa Fedha na Waziri wa Elimu.
Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Ouattara wamezungumzia hali ya elimu bara la Afrika na Ivory Coast kwa ujumla na haja ya kufanya mageuzi makubwa katika elimu ili kuweza kuendana na kasi ya nchi zilizoendelea.
Rais Mstaafu Kikwete amempongeza Rais Outtara kwa jitihada kubwa anayoifanya kuinua elimu nchini mwake. Kwa mujibu wa utafiti wa Kamisheni, Ivory Coast iko katika nafasi nzuri ya kufikia viwango vya juu vya ubora wa elimu vya nchi zilizoendelea iwapo itaongeza juhudi ya kufanya mageuzi kulingana na mapendekezo ya Kamisheni hiyo.
Rais Outtara amemuhakikishia Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete azma ya nchi yake kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu nchini mwake. Ameelezea utayari wa nchi yake kujiunga na mpango huo wa kufanikisha mapinduzi ya sekta ya elimu ndani ya kizazi kimoja ifikapo mwaka 2040.
Akiwa jijini Abidjan, Rais Mstaafu ametembelewa na viongozi wa Watanzania wanaofanya kazi Benki ya Maendeleo ya Afrika na Watoto  wa Watanzania hao ambao walitaka kujua kuhusu masuala ya uongozi na maisha baada ya kustaafu. 
 Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu  Dkt. Jakaya Kikwete akikaribishwa na Rais Alassane Ouatara wa Ivory Coast jijini Abidjan katika Ikulu ya nchi hiyo.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akimkabidhi ripoti ya 'Kizazi cha Elimu' Rais Allasane Ouatarra wa Ivory Coast
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mazungumzo na Rais Alassane Ouattara. Kulia kwake ni Makamu wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Daniel Kablan Duncan
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiagana na Rais Alassane Ouattara baada ya mazungumzo yao   Ikulu ya Ivory Coast.

 Rais MStaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Uongozi wa Watanzania wanaofanya kazi Benki ya Maendeleo ya Afrika jijini Abidjan
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia mazungumzo na baadhi ya watoto wa Watanzania waishio Ivory Coast waliomtembelea hotelini kwake Abidjan
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiwasainia autograph  watoto waliomtembelea hotelini kwake  jijini Abidjan

24 February 2017

WAKAMATWA KWA KUJIHUSISHA NA KILIMO CHA BANGI WILAYANI NGARA NA BIHARAMULO

Jeshi la polisi katika wilaya za Ngara na Biharamulo mkoani Kagera linawashikilia wakazi watano wa wilaya hizo kwa kujihusisha na kilimo cha bangi ambayo ni madawa ya Kulevya huku wakihusika kuharibu mazingira ya misitu.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Agustino Olomi amethibitisha kukamatwa kwa watu hao, ambao walikamatwa kwenye operesheni ya kukamata wanaojihusisha na kilimo cha bangi wiki hii pamoja na watumiaji au wafanya biashara wa madawa ya kulevya katika mkoa wa Kagera
Kamanda Olomi aliwataja waliokamatwa kwenye wilaya hizo ni Fabian Kasigo (45), mkazi wa Kazingati, Ndaluhekeye Chiza (37),Nestory Kachukuzi 42), Renatus James (44) Khalid John (33) wakazi wa wilaya ya Ngara na James Maliatabu (35) mkazi wa kata ya Nyantakara wilayani Biharamulo.
Mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele alisema katika msako wa kuwakamata wakulima wa bangi wilayani Ngara jumla ya mashamba ekari 20 yalibainika na wakulima wa zao hilo wanalilima katikati ya mapori wilayani humo
Mntenjele alisema wakulima waliokamatwa na kuhojiwa walidai wanauz zao hilo kati ya Sh15,000 hadi Sh 17 000 kwa wateja kutoka nchi jirani za Rwanda na Burundi na kwamba wanalima zao hilo wakikata miti kwenye vyanzo vya maji
“Wanapolima bangi wanaiweka katikati ya mashamba ya mahindi na huwezi kutambua kwani wanatembea umbali mrefu katikati ya mabonde yanye vyanzo vya maji na kukata miti kisha kupanda kupanda bangi hiyo”Alinema Kanali Mntenjele
Alisema katika msako uliofanyika kwa siku tatu wilayani Ngara kata ya Ntobeye, Keza kiasi cha ekari 20 zilibainika, wanaolima zao hilo wakiwatumia hata wahamiaji haramu kutoka mataifa jirani na wilaya hiyo wakiishi porini na kuletewa mahitaji ya chakula.
Aidha mkuu wa wilaya ya Biharamulo Saada Malunde alisema kata iliyofanyiwa msako kukamata wakulima wa bangi ni kata ya Nyantakara na Nemba ambapo mkulima mmoja James Maliatabu (35) alikutwa na shamba la bangi ekari 10.
Alisema vita ya dawa za kulevya kwa maeneo ya vijijini ni utumiaji wa bangi ambapo pia kamati za mazingira katika vitego na idara za halmashauri zinatakiwa kuunga mkono serikali kuwataja na kuwakamata wanaojihusiha na biashara ya madawa ya kulevya ili kufikishwa kwenye vyombo vya sheria
Pia baadhi ya wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama katika wilaya hizo walishauri serikali za vijiji na madiwani hata maafisa kata na tarafa kufanya zoezi la kuwasaka wakulima wa bangi kila mahali ili kutokomeza madawa ya kulevya kote nchini.
 Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya ngara mkoani kagera ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo Luteni Kanali Michael Mtenjele wakisafiri kwa pikipiki kuelekea kwenye mashamba ya kilimo cha bangi kata ya Keza tarafa ya Rulenge ambapo Jumla ya ekari 20 zimebainika na kukamatwa watu wanne wanaojihusisha na kilimo cha bangi katika mapori pamoja na misitu yaliyoko kitongoji cha Mulole kata hiyo ya keza 
Mwenye chupa ya maji na sweta la bluu ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ngara Aidan Bahama ambapo alilazimika kutambaa akishuka na kupanda milima kuingia ndani ya mashamba ya bangi 
Picha na habari by Shaaban Ndyamukama
 BOFYA HAPA KUDOWNLOAD BUKOBAWADAU APP Kwa habari mpya za uhakika kilahisi zaidi kwa kudownload Application ya Bukobawadau kwenye simu yako kutoka play store

AJALI YAUA WATU WANNE MJINI BUKOBA


WATU wanne wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa kufuatia ajari ya gari iliyotokea kata Rwamishenye manispaa ya Bukoba mkoani Kagera  
Hayo yamebainishwa na kamanda wa polisi Augustin Ollomi wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa hari juu ya tukio hilo. Hata hivyo alisema kuwa ajari hiyo ilitokea tarehe 24 mwaka huu majira ya saa 16 .30 jioni katika barabara ya Uganda maeneo ya Rwamshenye wakati gari lililosababisha ajali hiyo lilikuwa na no za usajiri T.377 BZW aina ya EICHE likiwa linaendeshwa na Josiah Joel Kasigwa (47) mkazi wa miembeni manispaa ya Bukoba. Aliwagonga waendesha pikipiki Damian Augustno (30) mhaya aliyekuwa na pikipiki namba MC .188 AZM aina ya bajaji boxer Denis (32) mhaya mkazi wa Rwamishenye alikuwa na pikipiki namba MC.582 aVQ aina ya Sanlg Alisema kuwa watembea kwa mguu waliogongwa ni Patricia Patrick (35) mfanyabiashra na mkazi wa Rwamishenye, Florence Innocent (28) nakusababisha vifo vyao papo hapo. 

 Tukio hilo Iilitokea wakati gari hilo lilipokuwa likitoka shule kuchukua wanafunzi na kuwapeleka majumbani kwao.  Aliwataja majeruhi kuwa Jackson Sebastian (10) Leus Optati (12) Molin Sebastin (8) ,Johansen Chrizostom (11) Kelvin Clemence (9) ,Wema Idrisa (36) wate wanafunzi Aidha Ollomi alisema kuwa majeruhi hao wametibiwa na kuruhusiwa isipokuwa Jackosn Sebastian amelazwa na hali yake inaendelea vizuri, Na, mtuhumiwa amekamatwa na jeshi la polisi na chanzo cha ajali kinachunguzwa.  

Naye Katibu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa kagera Kilwanila Kaiza alikili kupokea miili ya watu wane waliopoteza maisha na kuhifadhiwa katika mochwali iliyopo katika hospitali ya Rufaa iliyopo mjini Bukoba.
  Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajari hiyo rwehumbiza Belezeti ,atwaa mickdard alisema kuwa gari iliyosabisha ajari ni gari la shule ya msingi na awali ya kujitegemea Rwekiza.  "Tuliona gari inakuja kasi Sana mi nikamwambia mwenzangu kuwa unaona ngoma hiyo toka toka tukakimbia Mara baada ya muda ikagonga mti wa mbele basi ikaanguka"alisema belezet  "Sema tu watu sio wasikivu alipiga Sana honi lakini watu hawakujari wakaendelea tu kufanya mambo yao hadi gari inawafikia Walikuwa wamekaa ndo kufikia hali hiyo ilitokea"alisema mickdard. 
Pata habari mpya za uhakika kilahisi zaidi kwa kudownload Application ya Bukobawadau kwenye simu yako kutoka play store BOFYA HAPA KUDOWNLOAD APP

WEMA SEPETU AONGEA NA WANAHABARI  ATANGAZA KUAMIA CHADEMA

"Nilipokua kada, nilijitoa muda wangu na maisha yangu. Lakini, nilivyotegemea havikutokea. Sisemi nilitaka kubebwa au la" - Wema Sepetu "Nilizaliwa na kulelewa ndani ya Chama Cha Mapinduzi. Baba yangu alikua kada na alipofariki nadhani aliniachia ukada" - Wema Sepetu .

"Kama nimechukua hata shilingi elfu kumi toka chadema, naomba kaburi la baba yangu lititie kule Zanzibar" -Wema Sepetu "Nimeonewa na nimefanywa nijisikie mnyonge ndani ya chama. Mapenzi ni nipe nikupe, yakiwa ya upande mmoja sio mapenzi"-Wema Sepetu "Nimekuwa nikipewa ushauri & kuonywa kuwa nitafanywa vibaya, nisifanye hivi. Nimeshavaa magwanda sasa, nipo tayari kupigana"-Wema Sepetu  
"Natamka rasmi nimeamua mwenyewe kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenda CHADEMA"- Wema Sepetu "Ni kweli mimi na Wasanii wenzangu tunaidai pesa nyingi CCM. Tukifuatilia tunaambiwa tukamdai Kikwete."- Wema Sepetu

TETEMEKO LA ARDHI RUKWA

 TETEMEKO RUKWA: Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 5.7 limetokea huko Sumbawanga mkoani Rukwa usiku wa kuamkia leo, RPC George Kyando asema hakuna madhara yaliyoripotiwa #GazetiNiMwananchi

RAIS MSTAAFU ALHAJ ALLY HASSAN MWINYI KATIKA SHEREHE YA UHURU WA KUWAIT USIKU HUU JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akipokea zawadi ya mchoro toka kwa Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Andrew Mahiga
  Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akikata keki na  Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Andrew Mahiga
 Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akikata keki na  Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Andrew Mahiga
Keki ya hafla hiyo  ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. 
Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akiwa katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kulia kwake  ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Andrew Mahiga.
 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU